Frash votex

Translate

Tuesday, 10 June 2014

Wabaguzi ndio wanapinga Qatar


Rais wa shirikisho la kandanda duniani, FIFA, Sepp Blatter.
Mkuu wa shirikisho la kandanda, FIFA, Sepp Blatter amesema madai ya rushwa katika uchaguzi wa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022 yamechochewa na hisia za ubaguzi wa rangi.
Alisema haya alipokuwa akijibu madai yanayorushiwa baadhi ya wanakamati wa Fifa waliohusika na uchaguzi huo, wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa.



Blatter ameyasema hayo huko Sao Paulo, Brazil alipokuwa akizungumza na maafisa wa kandanda kutoka Afrika ."Kuna kimbunga kimeelekezewa Fifa tangu iichague Qatar. Inasikitisha sana kwamba yote yamechochewa na hisia za ubaguzi hasa wa rangi" Sepp BLATTER amenukuliwa kusema.
Ameahidi Fifa itakabiliana na chochote kinachobeba hata chembe ya kibaguzi.
Hata hivyo Fifa imeamua kufanya uchuguzi wake na imesema italiamulia swala hilo kati ya Septemba na October.
Katika kikao chao huko Sao Paulo, shirikisho la soka barani Afrika (CAF) nalo lilitoa cheche zake kwa vyombo vya habari vya kimataifa hasa magazeti ya Uingereza likisema ndio yaliyoanza kampeni hiyo dhidi ya Qatar na ya kuchafua jina la shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment