Inaaminika watu 27 wakiwemo watoto na wanawake wameuawa katika mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Walioshuhudia mapigano hayo wanasema kuwa miongoni mwa waliouawa walikuwa wanawake 14 na watoto 8 baadhi yao wakiwa ndani ya kanisa ambamo walikuwa wanalala
Waathiriwa wote walikuwa watu wa kabila la Bafuliru.
Haijulikani nani aliyetekeleza mashambulizi hayo lakini eneo hilo limeshuhudia mgogoro kati ya watu wa kabila la Bafuliru na Barundi.
Mwandishi wa shirika la habari la Reuters alisema kuwa waathiriwa walipigwa risasi , kudungwa visu au kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba zao.
No comments:
Post a Comment